Students Corner
![Picha](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgX3r6PzJrJf_8hH2qQEZeH0xeNjc3tUE19agXc0uvTiNqG8QDoeEeRj5aM3Q_UjF46BGDZjwmcROTFB2cLOIqUX1H27b2UqUgauhKgNzrPh9LPlADhA0vKQxi_moYtJmltbqXc1REpdcpS/s1600/poster_2021-11-12-083051.png)
Kila mzazi angependelea mwanae afanikiwe katika masomo na kufaulu mitihani yake. Pia kila mwanafunzi anahitaji KUFAULU katika mitihani yake. Walimu nao hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika mitihani yao. KUFAULU mtihani ni muhimu kwa malengo ya mwanafunzi, kwani anaposhinda mitihani humwezesha kuwa na mtazamo wa juu kielimu, kwa mfano KUPATA CHETI , DIPLOMA AU DIGRII , kitu ambacho humfanya afae kwenye KAZI. Wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwa baadhi ya WANAFUNZI kumudu MASOMO na mitihani yao. WAKATI HUO HUO wapo baadhi yao ambao wao KUFAULU MITIHANI si tatizo Sasa mtu anaweza kujiuliza , kwa nini WANAFUNZI wengine WASHINDWE na wengine WAFAULU vizuri katika Masomo NA MITIHANI yao ? MAFANIKIO katika MASOMO na KUFAULU MITIHANI kunahitaji UWEZO WA ASILI, KUFANYA KAZI KWA BIDII na KUFUATA KANUNI NA MBINU ZA KUSOMA. Wanafunzi wengine huona ugumu katika MASOMO...