Ujasiria mali na Maisha
![Picha](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEierCgwhmqLzvYUIqmMkH6_-Efr92AL7Oh1-tD0QHVJbjkJbxcGXQxsgQodHF85Jb7vyj_h-9XqYRwRWNZXaCAhUy3tWx8pNxsdjHFVwer_AbO4gdJJMsWcTzkRkuJMuHaoGzeZYT55_rfi/s1600/poster_2021-10-04-074005.png)
Wewe ni mjasiria mali? Au ungependa kuwa mjasiriamali? kama wewe ni mjasiriamali au ungependa kujifunza ujasiria mali tafadhali fuatilia ukurasa huu ili unufaike zaidi kuhusu ujasiria mali na maisha kwa ujumla. UJASIRIA MALI NA MAISHA Neno ujasiriamali lilianza kutumika miaka ya 1700 likiwa na maana ya kawaida ya kuanzisha biashara. Lakini wachumi wao wana maana zaidi ya hii. Kukabiliana na vikwazo vya biashara endapo kuna uwezekano wa kupata faida. Kwa wengine ni kuwa na uwezo wa kukwepa vikwazo vya biashara ili ufanikishe biashara yenye faida. Pia wengine wamemuelezea mjasiriamali kama ni mtu mbunifu mwenye uwezo wa kuuza ubunifu wake. Wachumi wengine wameendelea kumuelezea mjasiriamali kama mtu mwenye kuleta bidhaa au huduma za kibunifu kwenye soko ambazo hazijawahi kuwepo. Katika karne ya 20, mchumi mmoja kwa jina Joseph Schumpeter (1883-1950) alifafanua kuwa mjasiriamali ni mtu mwenye kuleta ubunifu na maboresho yenye kuleta sio tu hamasa bali pia kuwa ...