Hamasa za Maisha
Hizi ni Nukuu ( Quotes ) zinazoweza kukuhamasisha Katika kufikia ndoto zako, Binafsi hunipa Ari na Moyo wa Kufanya kazi kwa bidii ili kuyatimiza malengo yangu, natumaini na wewe zinaweza kuwa Kichocheo Kikubwa cha mafanikio kwako pia. 1.Muujiza uliopo kwenye kufanikiwa ni kuacha kutamani na kuanza kutenda. By J. Kweka 2.Usikubali uoga wako uamue hatima ya maisha yako. 3.Anguka mara NANE lakini simama mara ya TISA. Chinese Proveb. 4.Ujasiri siyo Kutokuwepo kwa HOFU , bali ni kufanya kitu ingawa kuna HOFU . 5.Ukitaka kushindwa kufika unakokwenda ni kujaribu kumtupia jiwe kila mbwa anaye kubwekea njiani.By Winston Churchhill. 6.Furaha ya Maisha siyo kuwa na pesa nyingi, bali ni kuona pesa yako inasaidia wale wasiyojiweza. 7.Usipende kufanya mambo makubwa sana, Bali fanya yale madogomadogo kwa ufanisi mkubwa. By St. Theresa of Calcutta. 8.Huwezi Kufanikiwa mpaka upende kazi ile unayoifanya. By Dale C...