Hamasa za Maisha
Hizi ni Nukuu (Quotes) zinazoweza kukuhamasisha Katika kufikia ndoto zako, Binafsi hunipa Ari na Moyo wa Kufanya kazi kwa bidii ili kuyatimiza malengo yangu, natumaini na wewe zinaweza kuwa Kichocheo Kikubwa cha mafanikio kwako pia.
1.Muujiza uliopo kwenye
kufanikiwa ni kuacha
kutamani na kuanza
kutenda. By J. Kweka
2.Usikubali uoga wako
uamue hatima ya maisha
yako.
3.Anguka mara NANE
lakini simama mara
ya TISA.
Chinese Proveb.
4.Ujasiri siyo Kutokuwepo
kwa HOFU, bali ni
kufanya kitu ingawa
kuna HOFU.
5.Ukitaka kushindwa
kufika unakokwenda ni
kujaribu kumtupia jiwe
kila mbwa anaye
kubwekea njiani.By
Winston Churchhill.
6.Furaha ya Maisha siyo
kuwa na pesa nyingi, bali
ni kuona pesa yako
inasaidia wale
wasiyojiweza.
7.Usipende kufanya
mambo makubwa sana,
Bali fanya yale
madogomadogo kwa
ufanisi mkubwa. By
St. Theresa of Calcutta.
8.Huwezi Kufanikiwa
mpaka upende kazi ile
unayoifanya.
By Dale Carnegie.
9.Ukitaka kufanya
mabadiliko makubwa
katika maisha, acha
kuangalia ukubwa wa
tatizo lako.
By T. Harv Eker.
10.Watu wengi hawaishi
ndoto zao, kwa kuwa
wanaishi uoga wao.
By Les Brown
11.Usiache yale usiyoweza
kufanya yaingilie na
yale unayoweza
kufanya.
12.Ni bora kufeli katika
uhalisia kuliko kufaulu
katika kuiga. By Herman
Melville.
13.Vitu vingi vya maana
katika Dunia vilifanywa
na watu ambao walizidi
kujaribu hata pale
mambo yalivyoonekana
yameshindikana kabisa.
Dale Carnegie.
14.Haijawahi kuchorwa
mahali popote picha ya
kuvutia ya mtu mvivu.
By Oprah Winfrey.
15.Mafanikio yako
hupimwa kwa ukubwa
wa vikwazo ulivyopitia
Kufikia Malengo
yako. By J. Kweka.
16.Inakupasa kuamka kila
asubuhi na hamasa,
kama unataka kulala
usiku ukiwa
umeridhika. By George
Lorimer.
17.Hamasa ndiyo
inayokufanya uanze
safari yako ya
mafanikio. Tabia ndiyo
inayokufanya uendelee
mbele katika mafanikio.
By Jim Ryun.
18.Uoga wetu katika
maisha usiwe katika
kushindwa, bali katika
kushinda vitu visivyo na
maana. By Francis Chan
19.Akili ndogo hushikwa
na kutishwa na hali
ngumu, Wakati Akili
kubwa huvuka na
kupanda
juu ya matatizo.
20.Inaweza ikakubidi
kupigana katika vita
zaidi ya mara moja ili
ushinde.
21.Mafanikio siyo
kutokufanya makosa,
Bali ni kuhakikisha
hurudii kosa ulilolifanya
zaidi ya mara moja. By
George Bernard Shaw.
22.Uwekezaji mzuri ni ule
wa kuwekeza katika
Maarifa, kwani
matunda yake
utayafaidi daima.
By Warren Buffett.
23.Kama unaweza
kuhesabu hela zako,
Basi inakubidi ufanye
kazi kwa bidii sana.
By Genius Ginimbi.
24.Kuzaliwa masikini si
kosa lako, Bali kufa
masikini ni kosa lako.
By BillGate.
25.Kupata 0 katika
mtihani haimaanishi
huwezi, ni kwamba una
njia nyingine 100 za
kufanya vizuri zaidi.
By J. Kweka.
26.Muda mzuri wa
kupanda mti ni miaka
10 iliyopita, lakini muda
mwingine mzuri zaidi ni
sasa. Chinese Proverb
27.Kitu pekee
kinachokutenganisha
wewe na mafanikio
yako ni Fikra na
mtazamo wako.
28.Kuwa hodari kusimamia
kile unachoamini hata
kama ukiishia
kusimama mwenyewe.
29.Ni bora kujaribu na
kushindwa, kuliko
kutojaribu kabisa,
By Roy T Bennet.
30.Mtu pekee ambaye
hajawahi kukosea ni
yule ambaye hakuwahi
kujaribu kitu kipya.
31.Kuna Wakati utafika
utagundua muda wa
kufanya yale Mambo
Uyapendayo ulishapita,
Lakini wakati mwingine
mzuri ni sasa.
32.Hujachelewa kuwa yule
unayetamani kuwa.
33.Kula chakula kama
dawa kwa ajili yako;
Vinginevyo utakuja
kula dawa kama chakula
chako. By Michael Osae
34.Mafanikio ni jumla ya
nguvu kazi ndogondogo
zinazorudiwa kila siku.
By Robert Collier.
35.Mwanzo wa Kila
Mafanikio ni njaa na kiu
ya hayo mafanikio.
By J. Kweka.
36.Usisubiri fursa itokee,
Bali Tengeneza fursa
yako mwenyewe.
By Chris Grosser.
37.Wajasiriamali wenye
mafanikio ni watoaji na
si wachukuaji.
38.Vitu vizuri huja kwa
mtu yule anayevisubiri,
Lakini Mafanikio huja
kwa mtu mwenye
kutoka nje na kuyafuata.
39.Kama uko tayari
kufanya kazi kwa nguvu
zaidi ya unavyolipwa,
Mwishowe utalipwa
zaidi ya kazi
unayofanya.
By J. Kweka.
40.Mafanikio ni
kinachokuja baada ya
kuacha kujipa
vijisababu.
By Luis Galarza.
41.Akili yako ina nguvu
kuliko unavyodhani,
Jaza akili yako na
maneno na fikra
chanya na utaona
Mafanikio yake.
42.Ili Ufanikiwe, inakubidi
Ujaribu kufanya kitu
kimoja kila siku
kinachokutisha.
43.Mafanikio
yameungwa na
mipango.
Na ukishindwa kupanga,
Umepanga kushindwa.
By John Beckley.
44.Ukitaka kuwa wa
thamani, tengeneza
thamani kwa wengine
Kwanza. By J. Kweka.
45.Jifunze Elimu zote,
Lakini Elimu ya fedha
ina Umuhimu Wake.
By J. Kweka.
46.Katika Maisha Kuna
siku mbili tu muhimu,
nazo ni Siku ya
kuzaliwa na ya pili
ni Siku ya Kujua
kwanini Ulizaliwa.
By J. Kweka.
47.Ukitaka kuwa mtu wa
mafanikio, Kuwa makini
sana na kitu Ulacho,
Usomacho, Uangaliacho
na Marafiki
wanaokuzunguka.
By J. Kweka.
48.Ukitaka kumla tembo
usiangalie ukubwa
wake, Na ukitaka
kufanikisha jambo
Anza kidogokidogo.
49.Vita vya kwanza
vinavyomtesa binadamu
ni hofu, na vya pili ni
kukata tamaa.
By J. Kweka
50.Wengi tunatamani
kusikia kisemwacho,
lakini hatuna mbinu za
kusikiliza. By J. Kweka.
51.Usikimbilie Pesa, bali
penda kile
unachokifanya na
kifanye kwa ufanisi
mkubwa nayo pesa
itakukimbilia.
By Samantha Wills.
52.Kufanikiwa ni kama
fumbo, Ukiona Maisha
yanakupa Limao; Wewe
tumia hizo limao
kutengenezea juisi.
By J. Kweka.
53.Ukipewa masaa
Matano kukata mti,
Tumia masaa matatu
kunolea Shoka.
By Abraham Lincoln.
54.Linda sana mdomo
wako, Ukiufungua ujue
Unaiambia dunia kuwa
wewe ni mtu wa aina
gani.
By Les Brown.
55.Tunapata afya kwa kula
vyakula, na tunapata
maarifa kwa kusoma
vitabu. By J. Kweka.
56.Ili kufanikiwa, katika
kamusi yako futa neno
"Haiwezekani"
By Napoleon Hill.
57.Fursa ni kama embe,
wakati unasubiri liive,
wengine wanalila kwa
chumvi. By J. Kweka.
58.Ukiacha kusoma Vitabu,
ujue usha anza kufa
taratibu. By J. Kweka.
59.Usipojiajiri kwenye
kutimiza ndoto zako,
Basi utaajiriwa kutimiza
za mwenzako.
60.Kuwa wa kwanza
kujaribu na kushindwa,
ili upate muda mzuri wa
kujifunza. By J. Kweka.
61.Kiongozi Bora ni
msomaji mzuri wa
Vitabu.
62.Silaha nzuri ya
kutokukosolewa ni hii,
Usijaribu chochote,
Usianzishe chochote, na
Usifanye chochote.
By J. Kweka.
63.Katika kukamilisha
safari yako ya mafanikio,
Jifunze kukaa kimya.
By J. Kweka.
64.Ubunifu ndiyo ajira
pekee ya Kudumu,
Kwa hiyo heshimu
ubunifu wako.
By J. Kweka
65.Siri ya Mafanikio yetu
ni kutokukata tamaa.
By Wilma Mankiller.
66.Uzoefu ni Kufanya
Makosa na kujifunza
kutokana na Makosa
hayo.
By Bill Ackman.
67.Usiogope kuanguka,
Bali ogopa sana kubaki
ulipoangukia.
By J. Kweka.
68.Kanuni ya Maisha iko
hivi "Ukitaka kupata
unachotaka, Saidia
wengine kupata
wanachotafuta".
By J. Kweka.
69.Ili kufanikiwa tumia
kanuni hii:-
Mipango+Pesa+Uwekezaji=Mafanikio.
70.Kama biashara yako
haina changamoto basi
mafanikio yake ni
madogo.
By Winston Churchill.
71.Elimu si njia ya
kuepukana na umaskini,
Bali ni njia ya
kupambana na
Umaskini.By J.K Nyerere.
72.Kabla hujajiona hufai,
tambua kuna watu
wakikutazama
wanajivunia.
73.Ujuzi na maarifa havina
thamani kama
havitawekwa kwenye
matendo.
By J. Kweka
74.Ukitaka kushinda
katika mbio kimbia na
wenzako. Ila ukitaka
kufika mbali zaidi
kimbia mwenyewe.
75.Hatukui wakati wa
utulivu, Bali tunakuwa
wakati wa changamoto.
76.Wakati wa njaa usiombe
samaki, Bali omba ujuzi
wa kuvua samaki ili
uweze kula kila siku.
77.Kuna Watu Mafanikio
Yao Huja Taratibu,
Lakini Unapomfanyia
Fitina Unamsaidia
Kuyafikia Mapema
Zaidi. By J. Kweka.
78.Ukiona Unashindwa
Kumdhibiti Adui Yako
Katika Nia Zake, Basi
Ungana Naye Kutimiza
Malengo Yake.
79.Kila Ng'ombe Hujua
Harufu Ya Mfugaji Wake,
Hata Mafanikio Huenda
Kwa Yule Mwenye Kujua
Kanuni Za Kuyapata,
80.Uwendawazimu
mmojawapo ni ule wa
kufanya jambo lile lile
kwa staili ile ile huku
ukitegemea matokeo
tofauti.
By Albert Eistein
81.Ukiona unakosolewa
kwa kile unachokifanya,
jua kabisa uko karibu na
mafanikio. By J. Kweka
82.Hakuna mtu aliyewahi
kuwa maskini kwa kutoa.
By Anne Frank
83.Furaha ya maisha yako
hutegemea ubora wa
mawazo yako.
By Marcus Aurelius
84.Haitoshi tuu kuwa na
akili nzuri, Bali jinsi
unavyoweza kuitumia
vizuri. By Rene Descartes.
85.Tunachojua ni tone,
Kile ambacho hatujui ni
bahari.
By Sir Isaac Newton
86.Ishi kana kwamba
utakufa kesho. Jifunze
kana kwamba ungeishi
Milele. Mahatma Gandhi.
87.Hekima pekee ya kweli
ni katika kujua hujui
chochote. By Socrates
88.Kushindwa ni kitoweo
kinachokipa mafanikio
ladha yake.
By Truman capote.
89.Fursa huzidisha kadri
zinavyokamatwa.
By Jua Tzu
90.Usihukumu kila siku
kwa mavuno unayovuna.
Bali kwa mbegu
unazopanda.
By Robert Louis
91.Hakuna rafiki
mwaminifu kama kitabu.
By Ernest Hemingway
92.Kwa maana ni katika
kutoa ndipo tunapokea.
Mtakatifu Francis wa Assisi
93.Sijashindwa, bali
nimepata tu njia 10,000
ambazo hazikufanya
kazi.
By Thomas Edison
94.Utajiri haumo katika
kuwa na mali nyingi,
Bali kwa kuwa na
mahitaji machache.
By Epictetus.
95.Hakuna chochote
kinachowezekana kwake
ambaye hatajaribu.
By Alexander the Great.
96.Kama hujasimamia
kwenye kitu chochote,
Basi chochote chaweza
kukuangusha.
By J. Kweka.
97.Kobe hutembea taratibu
lakini hajawahi kukosa
chakula chake.
By J. Kweka
98.Tembo ni mnyama
mwenye nguvu nyingi
lakini huangushwa na
sisimizi.
99.Tajiri akiugua maskini
huenda kumsalimia na
kumpa pole, lakini
maskini akiugua
husubiri hadi apone na
kwenda kwa tajiri kutoa
taarifa kuwa alikuwa
mgonjwa.
100.Masikini hata akitoa
mawazo mazuri kiasi
gani kwenye kikao
ataonekana
anasumbua, lakini
tajiri akitukana
kwenye kikao
ataonekana anafanya
utani.
101.Marafiki wakweli
hupatikana kipindi cha
shida lakini,
wanaopatikana kipindi
cha Mafanikio ni
wachawi.
By J. Kweka.
102.Nilikuwa najiuliza
Kwa muda mrefu
ulemavu wangu ni
Upi ndipo nikagundua
kuwa ni wa kutotambua
talanta yangu.
By J. Kweka
103.Kanuni ya mafanikio
Yako iko hivi:
Effort+Determination
+Prayer =Successful
104.Kwenye wingi wa
maji ni Mjinga tu ndiye
anaye weza kuwa na kiu.
Bob Marley
105.Mjasiriamali ni yule
mwenye kuona FURSA
ambayo wengine
hawaioni. By J. Kweka
106.Safari ya Maili 1000
huanza na hatua 1.
Chinese Proverb
107.Msomi ni yule
mwemye Uwezo wa
Kuoanisha kati ya Elimu
ya Darasani na ile ya
Mtaani. By J. Kweka
108.Ukiwa na Marafiki 9
ambao ni Vichaa
Tambua kabisa wewe ni
Kichaa wa 10.
By J. Kweka
109.Mtu hujichorea ramani
ya Maisha yake
mwenyewe, Kwa hiyo
ichore kwa umakini.
By J.Kweka
110.Ukitaka kuishi
usiogope kufa. Kwa
maneno mengine,
Ukitaka kufanikiwa
katika maisha yako,
Usiogope Changamoto.
By J. Kweka
111.Usinionee Huruma,
Kwani Maisha yangu
ni kafara ya Mafanikio
yangu. By J. Kweka
112.Hakuna Ufundi
mkubwa kama
Wakuishi na Watu
Vizuri kwenye hii
Dunia yenye Sauti
nyingi. By J. Kweka
113.Kwenye hii Dunia
jitahidi sana Hadithi ya
Maisha yako Isimuliwe
Vizuri. By J. Kweka
114.Ukiona Mke/Mme wa
Bosi wako anajifunza
kuendesha gari ujue
kuna Ajira ya Mtu iko
matatani, Kwa hiyo
kaa tayari kwa kila
badiliko linalotokea
kwani Maisha ndivyo
yalivyo. By J. Kweka
115.Jifunze Kuiona
Dhahabu hata kama
ipo kwenye Tope.
By J. Kweka
116.Hakiwezi kukamilika
kitu Chochote kama
hujakianza. Anza sasa
bado hujachelewa.
By J. Kweka
117. Tai ni ndege mwenye
Uwezo wa kuona
kitoweo hata akiwa
mbali, nasi tujifunze
kuziona FURSA hata
kama hazionekani.
By J. Kweka
118.Penye Miti hapana
Wajenzi, Lakini
hapakosekani Asali.
By J. Kweka
119.Ukitaka kupanda juu,
paheshimu sana pale
Unapokanyagia.
By J. Kweka
120.Kwenye harakati za
Mafanikio tujifunze
kutumia neno SISI
kwani MIMI
Hakufikishi popote.
By J. Kweka
121.Mtu 1 Mwenye
Ushawishi ni wa
Thamani sana kuliko
watu 100 Wenye
Matamanio.
By Zig Ziglar
122.Ewe Mwanafunzi Soma
kwa Bidii kwani Tako
Husinyaa na Kuisha.
By Unknown
123.Kinachoshindikana
kwa Mwenzio kwako
kinawezekana. Songa
mbele Usikate Tamaa.
By J.Kweka
124.Haijalishi mnasema
nini juu yangu, Bali
ninachojali ni
ninapata nini kwenye
Maisha yangu. Nasonga
mbele nyuma Mwiko.
By J. Kweka
125. Ukarimu ndiyo Lugha
pekee ambayo Kiziwi
anaweza kuisikia na
Kipofu anaweza
Kuiona.
By Mark Twain
126.Nilipokuwa mdogo
niliwatamani sana
Watu wenye Akili, Kwa
sasa nimezeeka
nawatamani Watu
Wakarimu.
By Abraham Heschel
127.Hakuna mtu ambaye
alishaumizwa Tumbo
kwa Kumeza Maneno
Machafu yaliyosemwa
na Wengine.
By Winston Churchill
128.Tuna Masikio Mawili
na Mdomo Mmoja ili
Tusikilize Zaidi kuliko
Kuongea. By Epictetus
129.Usikubali watu
Wanaofaidi Wema
wako Wakufanye
Uache kuwa Mwema.
By J. Kweka
130.Ukarimu wa kweli ni
ule wa kumsaidia mtu
kitu ambacho kamwe
hawezi kukulipa.
By Frank A. Clark
131.Ni bora kuwa Upinde
kwenye Wingu la
Mwenzako kuliko
kuwa Ukungu.
By Maya Angelou
132.Ulimwengu huu
umejaa watu wengi
ambao hawajali
Chochote; Bali wewe
kuwa mmojawapo wa
anayejali sana kwenye
huu Ulimwengu.
By J. Kweka
133.Hakuna aliyewahi
kupandisha heshima
yake kwa kushusha ya
Wengine. By J. Kweka
134.Ulimi wa Kulaumu ni
Balozi wa Moyo
Usiokuwa na
Shukurani.
By J. Kweka
135.Ukitaka kushinda
katika biashara yako
inakubidi ushinde na
wateja wako.
By J. Kweka
136.Rafiki mzuri ni yule
anayekunyanyua
wakati wengine
hawaoni kama
umeanguka.
By J. Kweka
Hamasika na hii Hapa:-
Jack Ma Quotes on Entrepreneurship
Nukuu zaidi za Maisha:-
Mbinu za Kuamsha hamasa ya kufanikiwa kwako:-
Umuhimu wa kuwa na pesa:-
Usikate tamaa bado una nafasi ya kufanikiwa Jackma:-
........................................................................................
Siri 101 za kukuwezesha kuwa na Mafanikio Maishani:-
Ili kufanikiwa Maishani fuata Ushauri huu:-
Siri 13 za Kufahamu kuhusu Pesa:-
Mbinu wanazotumia Matajiri kufanikiwa zaidi:-
Nini cha kufanya ili ufanikiwe katika Maisha?
Mbinu za kukuwezesha kutimiza ndoto zako:-
Mbinu za kukuwezesha kupata mtaji wa kuanzisha Biashara ya ndoto zako:-
Mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuanzisha Kampuni au Biashara:-
Makosa ya kuepuka wakati wa kutengeneza Nembo/Logo yako:-
JackMa ni nani?
Oprah Winfrey ni nani?
Ben Carson ni nani?
Historia na mafanikio ya BenCarson:-
Bill gate ni nani?
Elon Mask ni nani?
Fahamu Chanzo cha utajiri wa Mabilionea hawa:-
Orodha ya Mabilionea wa Kitanzania hii hapa:-
VIDEO ZA KUHAMASISHA:
Misingi 10 ya Fedha na Mafanikio:-
Kanuni za Mafanikio:-
Orodha ya Vitabu Muhimu Kwa Mjasiriamali:-
Vitabu ambavyo ni Muhimu kuvisoma kama Unataka kufanikiwa Kibiashara:-
UCHAMBUZI WA VITABU MBALIMBALI VITAKAVYO KUINUA KIUCHUMI:-
Think and Grow Rich:-
Eat that Frog:-
The Journey to Wealth:-
Financial Freedom:-
Think like a Success:-
Nasaha 25 za Kukuamsha Usingizini:-
KAMA UMEGUSWA NA UNGEPENDA SAPOTI KAZI YETU HII WAWEZA KUTUMA KIASI CHOCHOTE KWENYE NAMBA HII YA
M-PESA: 0753775158 - JOACHIM KWEKA
Barikiwa Sana
...............................................................
Asantee nsurii
JibuFutaAsante sana kwa hamsa hii nzuri Sana.
JibuFutaHakika Shakina ni Kisima cha maarifa.
Asante nsurii
JibuFuta