Nidhamu ya Pesa
Vitu vya Kuzingatia ili kuwa na nidhamu ya pesa: Mambo 12 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia ni haya:- 1 . Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara. Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake. 2 . Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako. Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani. Kama kuna mtu kakwambia, Flan njoo kesho nikulipe deni lako - Basi wewe usiende kukopa vitu dukani au kumuahidi mtu mwingine kumpa pesa ambayo na wewe umeahidiwa. 3. Kama unataka kuhifadhi/kutunza pesa, kila unapopata pesa usianze kuitumia kwanza kisha ukategemea kutunza kiasi kitakachosalia. Hivyo basi, ukipata tu pesa, weka pembeni kiasi unachodhani kinafaa kutunzwa/kuhifadhiwa kisha tumia kiasi kilichobaki. 4. Ukipata nafasi ya kuonana na mtu tajiri, kamwe usiombe pesa. Bali Omba ma...