Nidhamu ya Pesa

Vitu vya Kuzingatia ili kuwa na nidhamu ya pesa:

Mambo 12 katika pesa ambayo unapaswa kuzingatia ni haya:-


1. Usikope pesa ya riba ili
     uanzishe biashara. 
     Usitegemee pesa ya mkopo
     kuianzishia biashara, upate
     faida kisha uirudishe pesa ya
     mkopo na riba yake.

2. Usitumie pesa ambayo bado
    haipo mikononi mwako. 
    Wala usije ukamuahidi mtu
    kumpa pesa ambayo
    umeahidiwa mahali fulani.
    Kama kuna mtu kakwambia,
    Flan njoo kesho nikulipe deni
    lako - Basi wewe usiende
    kukopa vitu dukani au 
    kumuahidi mtu mwingine
    kumpa pesa ambayo
    na wewe umeahidiwa.

3. Kama unataka
    kuhifadhi/kutunza pesa, kila
    unapopata pesa usianze
    kuitumia kwanza kisha
    ukategemea kutunza kiasi
    kitakachosalia.
    Hivyo basi, ukipata tu pesa,
    weka pembeni kiasi
    unachodhani kinafaa
    kutunzwa/kuhifadhiwa 
    kisha tumia kiasi kilichobaki.

4. Ukipata nafasi ya kuonana
    na mtu tajiri, kamwe 
    usiombe pesa. 
    Bali Omba maarifa ya
    kutengeneza pesa kama yeye,
    tena kwa mtaji mdogo.
    Maarifa ndio mtaji wa kwanza.
    Unaweza kupewa/kusaidiwa
    pesa iwapo una mawazo 
    mazuri ya kuzalisha pesa. 
    Baadhi husema, 
  "Omba ndoano, usiombe samaki"

5.Usitunze mbegu badala ya
   kuipanda. Watu wengi 
   hufurahia pesa wanayolipwa
   /kuipata kisha wanaiweka
   benki au nyumbani bila
   kuiwekeza. Wekeza pesa 
   ili uzalishe zaidi. Usiogope
   kuingia hasara, kila
   aliefanikiwa alipoteza
   kwanza kabla hajafanikiwa.
   Wengi walipoteza muda, 
   pesa, afya na hata matumaini 
   ya kufanikiwa, ila kwa 
   uthubutu wao, mwisho wa 
   Siku walifanikiwa”

6.Kamwe usimkopeshe mtu 
    pesa ambayo unahisi
    hatorudisha. Unapomkopesha
    mtu huyo pesa, jiridhishe
    mwenyewe moyoni kuwa 
    kama hatoweza kulipa basi 
    deni lake-halitoathiri urafiki
    wenu. Ukihisi kwamba
    kushindwa kwake kulipa
    kunaweza kuathiri urafiki
    wenu, basi mshauri aende 
    benki akakope”

7. Usikubali kumdamini mtu
     ambae huna uhakika kuwa
     atalipa kile unachomdhamini.
     Kumbuka- dhamana maana 
     yake utawajibika iwapo
     atashindwa kulipa.

8. Epuka kutembea na pesa 
    nyingi ambazo hata huna
    matumizi nazo wakati huo. 
    Unaweza kujikuta unafanya
    matumizi ambayo hayakuwa
    kwenye ratiba sababu ya
    ushawishi wa pesa ya mfukoni.
    Ili kuepuka haya, tembea na 
    pesa uliyopanga kuitumia 
    katika safari yako.
    Pesa nyingine itunze 
    mahali pengine palipo 
    salama”

9. Epuka kutunza pesa mahali
    pasipo sahihi. Maeneo kama 
    kwenye soksi, sidiria, chini
    ya mto wa kulalia, chini ya 
    begi, kwenye kopo au hata
    kwenye begi la safari,
    si maeneo salama.
  ~Ni rahisi kusahau, kuibiwa 
    au kupoteza pesa zako.
    Ni bora ukatunza pesa
    kielektroniki; yaani benki au
    kwenye simu au kwenye pochi
    yenye kamba ngumu ya kuivaa
    mabegani au wallet ambayo
    inatosha kwenye mifuko imara 
    na yenye vifungo kwenye nguo
    zako hasa uwapo safarini.

10. Usitumie pesa kwa kitu
      ambacho hakikuwa kwenye
      ratiba yako.
 Jiulize kwanza kabla hujanunua, 
    "Bila kitu hiki, maisha 
     yataenda au lah?” Ukiona 
     maisha yataenda bila kitu
     hicho, acha kukinunua.
     Tabasamu kisha ondoka.

11. Matumizi yako ya pesa
      yasizidi pato lako.
     Unaweza kuwa una ndoto
     kubwa/matumizi makubwa
     ya pesa kuzidi pato lako.
     Unapaswa kuwa bahili 
      katika matumizi yako.
     Cheza na pato lako. 
     Fanya matumizi
     makubwa pale tu pato lako
     litakapoongezeka. Hii
     itakuepushia kushindwa 
     kufanya baadhi ya mambo
     ya msingi na kisha ukajikuta
     unaishia kwenye madeni
     makubwa. 

12. Una ndoto kubwa hapo
      baadae; labda kujenga
      nyumba, kununua gari, 
      kununua kiwanja, simu
      nzuri hata pikipiki.
      Usikurupuke, ukanunua 
      kitu cha ndoto yako sasa
      eti tu sababu umekipata 
      kwa bei ya punguzo.
      Usichanganye kati ya mahitaji
      ya baadae na ya sasa.
     Pesa unayotumia kutimizia 
     ndoto sasa itumie kwa mahitaji
     ya sasa. Ndoto ibaki kuwa
     ndoto. Hii itakuepushia 
     kuingia katika madeni au 
     kuishi kwa shida sababu ya
     tamaa. Jipange taratibu 
     kutimiza ndoto yako.


Mkopo ni nini?

Siri za kufahamu juu ya fedha:-
Ufahamu zaidi juu ya Fedha:-

Amri Tano za kupata fedha
Part One:-
Amri tano za kupata Fedha
Part two:-
Kanuni 12 za kupata pesa:-

Tujifunze kutoka kwa Warren Buffet namna ya kupata pesa:-

Tatizo la wengi si ukosefu wa pesa, bali ni namna ya kuitawala pesa:-
Namna ya kutunza hela:-
Nunua Assert na si Liability:-

Mambo usiyoyajua kuhusu Pesa:-
Sababu za kushika hela na kuishia kuwa maskini:-
Umuhimu wa kuwa na hela:-
Matumizi sahihi ya Pesa:-

Muone Dada aliyeacha kazi na kuwa Milionea:-

Mbinu za Kupanga Bajeti na kuweza kuwekeza kwa Haraka zaidi:-
Misingi 10 ya Fedha na Mafanikio:-

Sheria juu ya Uchezeaji wa Fedha nchini Tanzania:-

............................................................................



 

Maoni

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Shakina Pre and Primary English Medium School

Kikatiti Secondary School

Ujasiria mali na Maisha